Kwa mujibu wa mwakilishi wa mwanamuziki huyo, Jennifer Lopez hatashiriki sherehe za mwaka huu za ufunguzi wa kombe la dunia ambapo hajatoa sababu ya kufikia uamuzi huo.
Lopez aliungana na rapa Pitbull pamoja na nyota wa nchini Brazil Claudia Leitte kwa ajili ya kurekodi wimbo maalum wa kombe la dunia kwa mwaka huu uliopewa jina la “We Are One (Ola Ola).”
Wanamuziki hao watatu kwa pamoja walitakiwa kuimba wimbo huo katika sherehe za ufunguzi katika mechi ya kwanza lakini Jlo amesitisha na kusema hatokuwepo tena.
0 Response to "Jennifer Lopez ajitoa kufanya onyesho katika ufunguzi kombe la Dunia"
Post a Comment