Diamond Platnum kuachia video mbili kwa mpigo.

Diamond kuachia video mbili kwa mpigo, ni tofauti na alizowahi kufanya
Diamond Platinumz ametangaza kupitia Instagram kuwa ataachia video mbili kwa mpigo ikiwa ni siku chache baada ya kumalizana na BET Awards 2014.
Mashabiki wake wategemee kuona video mbili kwa wakati mmoja ambazo ni moja ya wimbo aliofanya na mkali wa Kukere, Iyanya wa Nigeria, na nyingine ya wimbo wenye asili ya ngoma za kitanzania Kitorondo aliyoipa jina la MdogoMdogo.
Diamond ameendelea kushare picha mbalimbali kutoka kwenye video hizo, picha zinazoashiria kuwa video hizo zitakuwa tofauti kabisa na video za awali za Diamond.
Katika moja ya picha alizoshare Instagram akiwa katika eneo lenye miamba na maporomoko ya maji huku akiwa amevaa kama mtu anaeishi nyikani, aliwataka mashabiki wataje uhusika wake.
“Nikikupa Nafasi moja tu ya Kunipa Jina katika Caracter hiyo we ungenipa jina Gani?..... [ If I was to give you a chance to give me a name from that character what would it be...?]”
KWA HABARI ZAIDI BOFYA/CLICK OLDER POSTS.
 BET Awards 2014's best perfomance from usher.

0 Response to "Diamond Platnum kuachia video mbili kwa mpigo."

Post a Comment