LUPITA NYONG'O ALA SHAVU LA FILAMU YA "STAR WARS"


Safari moja huanzisha nyingine, hii ndiyo inamtokea muigizaji wa kike kutoka Kenya Lupita Nyong’o ambaye ameendelea kupata mashavu makubwa tangu aonekane kwenye filamu ya 12 Years A Slave.
Lupita amechaguliwa kujiunga na waigizaji wengine wakubwa duniani katika filamu maarufu zaidi ya STAR WARS ambayo awali ilikuwa kipindi cha runinga.
Kwa mujibu wa BBC, mshindi huyo wa tuzo za Oscars anatarajiwa kuonekana katika kipindi cha msimu wa saba wa Star Wars ambayo itakuwa tayari na kuanza kuoneshwa kwenye majumba ya cinema kuanzia December 18, 2015.
Kipindi cha saba cha Star Wars kinasimamiwa na J.J Abrams na imetajwa kuwa filamu baada ya kufanya vizuri kama kipindi cha runinga kwa muda mrefu.
 

0 Response to "LUPITA NYONG'O ALA SHAVU LA FILAMU YA "STAR WARS""

Post a Comment