MUME WA FLORAH MBASHA AFUNGUA ATOBOA SIRI YA NYUMA YA PAZIA YA KUSINGIZIWA UBAKAJI

Upande wa pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza tangu ahusishwe na skendo ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na Uwazi katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa yake hiyo huku akitishia kujiua.

Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba anajua anachezewa mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.

ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar) si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”

KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”

MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00 asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa 3:00 hadi 4:00 usiku.

“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?

“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza kunifanya nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya yeye kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”

AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar), akampa semina ya kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na yeye awe huru.

“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari,  wakafoji majibu ya vipimo vikionesha kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya habari vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya kweli.

“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini. Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa uchungu.

HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu awe shahidi yangu.”

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu wametimiza miaka 12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth.

0 Response to "MUME WA FLORAH MBASHA AFUNGUA ATOBOA SIRI YA NYUMA YA PAZIA YA KUSINGIZIWA UBAKAJI"

Post a Comment