WAHINDI 14 WAMEKAMATWA DAR, WAMEINGIA KUFANYA BIASHARA HARAMU

Askari wa uhamiaji wamewakamata watu 14 katika maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam kutoka nchini India na Nepal ambao ni wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambapo watu hao wameingia nchini kinyume na taratibu za uhamiaji.

Kati ya watuhumiwa 14 watuhumiwa 12 ni wasichana ambao waliletwa nchini kwa lengo la kufanya maonyesho ya nyimbo za asili lakini wakajikuta wakingizwa katika biashara zingine ikiwemo kucheza muziki katika nyumba za burudani.

Kwa upande mtu anayedaiwa kuwaleta wasichana hao amesema amewaleta kwa lengo la kufanya maonyesho ya muziki huku akipinga kuwa wasichana hao hawatumii kinyume na hivyo.

Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mikoroshini msasani amewataka wakazi wa eneo hilo kujiepusha na tabia ya kukaa na wageni bila ya kutoa taarifa mamlaka husika.
Akithibitisha tukio hilo mkaguzi wa uhamiaji Bw Dotto Romana amesema wanawashikilia watu hao na watachukua hatua kulingana na mahitaji ya sheria.

0 Response to "WAHINDI 14 WAMEKAMATWA DAR, WAMEINGIA KUFANYA BIASHARA HARAMU"

Post a Comment