RAIA WA TUNDURU WAGOMBEA NYAMA YA KIBOGO ALIYEUWA MTU

 Wakazi wa wilaya ya Tunduru wakigawana  nyama ya Kiboko huku mmoja akimnyooshea mwenzie fimbo baada ya jamaa kutaka kuleta fujo wakati wa kugawana nyama hiyo.
Na Steven Augustino wa demashonews, Tunduru
WANANCHI wa Mji wa Tunduru Mkoani Ruvuma wamemuua  Kiboko aliye muua Mkazi wa Kitongoji cha Chacha katika Kijiji cha Mhuwesi katika kata ya Mhuwesi Tarafa ya Nakapanya Marehemu  Njaidi Selemani Njaidi (70) na kumla nyama yake bila kujali dini zao.

Katika kuonesha kuwa Mnyama huyo analiwa na waumini wa dini zote Maelfu ya wananchi walijitokeza kumlinda asitoke hadi usiku wa saa 9 walipotokea askali wa idara ya wanyamapori na kumpiga risasi. Aidha hali ilikuwa tete baada ya Kiboko huyo kuuawa ambapo mamia ya vijana wenyeguvu walijitokeza na kujitosa katika bwawa hili na kuanza kumshambulia kwa kutakata nyama hiyo huku wakiwa wanagawana na mwisho kikaja Kivutio amakioja cha kuwatishia visu askari wa idara hiyo na kuwapora ndoo 8 za nyama hiyo ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kuondoka nayo .

Kiboko huyo ambaye alimuua Marehemu Njaidi April 20 mwaka huu wakati akijaribu kukata kitoweo cha nyama baada ya kumkuta akiwa amelala katika eneo la shamba lake katika eneo la Mto Muhuwesi aliuawa na Askali wa Idara ya Wanyama pori katika eneo la Mto Nanjoka mjini hapa baada ya Wananchi hao kumzuwia asitoke katika bwawa lililopo kandokando yam to huo kwa zaidi ya masaa 20.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema kuwa walilazimika kumzuwia na kutomruhusu kutoka Kiboko huyo hadi auawe zikiwa ni juhdi za kuepusha madhara ambayo angeweza kuwafanyia wananchi amabo hupita katika njia ya eneo hilo wakiwemo wanafunzi wanaosoma katika Shule ya sekondari ya Kangoma mjini humo. 

Akizungumzia tukio hilo Mtendaji wa kata ya Nanjoka Said Mailon alisema kuwa Kiboko huyo alifika katika eneo hilo akiwa anatokea katika eneo la Mto Mhuwesi ambako alitembea kwa kufuata mto huo na hatimae akaingia katika mto masonya na kufanikiwa kuingia katika Mto nanjoka ambako alifia.

Alisema wakati Koboko huyo akiwa katika eneo la tukio wananchi hao walimshtukia baada ya kuona Nyayo za Miguu yake aliyokanyaga wakati akishambulia Mbogamboga katika Bustani zao hali ambayo iliwafanya watoe taarifa kwa uongozi wa idara ya Wanyamapori wakiwa wanaomba msaada wa kuuawa kwa kiboko huyo ili asiweze kusababisha madhara kwao.

 Akizungumzia tukio hilo afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya hiyo Bw. Jafeth Mnyagala pamoja na kukiri kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa baada ya kiboko huyo kuuawa na askari wenye silaha baada ya kupokea taarifa za kuwepo kwake katika eneo hilo.

Aidha alilaani vikali kitendo kilichofanywa na wananchi hao cha kuwapora Nyama na Ngozi na kugawana kwa ajili ya kitoweo hali ambayo alisema kuwa endapo askali hao wangepaniki wangeweza kusababisha madhara kwa Wananchi hao.

Bw. Mnyagala aliendelea kueleza kuwa matukio ya Viboko na tembo kuvamia na kufanya uharibifu katika mashamba ya wakulima wa Wilaya hiyo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kwamba kutokana na hali hiyo idara yake imekuwa ikifanya kazi ya ziada kuwafukuza wanyama hao ili wasiendelee kuharibu mazao ya watu.

 Alisema pindi inapo bainika kuwa Viboko na Tembo hao wanazidi kufanya mashambulizi ya kudhulu Watu ama kufanya mauaji kama ilivyo tokea idara hiyo pia imekuwa ikichukua hatua za kuwasaka na kuwaua Wanyama hao haraka iwezekanavyo  ili wasiendelee kusababisha madhara kwa watu wengine.

0 Response to "RAIA WA TUNDURU WAGOMBEA NYAMA YA KIBOGO ALIYEUWA MTU"

Post a Comment