MSAKATA KABUMBU BALOTELLI AMVALISHA PETE MPENZI WAKE

Mario Balotelli akiwa na mpenzi wake, Fanny Neguesha.
 Mpenzi wa Mario Balotelli, Fanny Neguesha.
MSHAMBULIAJI wa Italia na AC Milan, Mario Balotelli ametangaza kumchumbia mpenzi wake, Fanny Neguesha kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya England mjini Manaus.
Mchezaji huyo mtata wa AC Milan amethibitisha hilo katika ukurasa wake wa Instagram kwa kuposti picha ya mkono wa mpenzi wake huyo ikiwa na pete ya uchumba jana jioni.
Balotelli ameambatanisha picha na ujumbe usemao: "Amesema ndiyo.. Ndiyo muhimu zaidi katika maisha yangu. Hilo ndilo lilikuwa swali langu! Nakupenda, na furahia siku ya kuzaliwa kwao pia! Je t'aime my WIFE'.

0 Response to "MSAKATA KABUMBU BALOTELLI AMVALISHA PETE MPENZI WAKE"

Post a Comment