PROFESA JAY AFANANISHWA NA VASCO DA GAMA

Profesa kuachia albam ya
Kipi Sijasikia’ ni wimbo mpya wa Profesa Jay ambao tangu uingie mitaani na radioni umeendelea kupata nafasi kubwa na kueleweka haraka kwa jinsi wimbo huo ulivyo na ujumbe unaoyagusa maisha ya watanzania wengi.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, msanii huyo mkongwe amesema wimbo huo aliomshirikisha Diamond Platinumz ni wimbo wa kwanza kutoka kwenye albam yake mpya aliyoipa jina la ‘The Icon’.
Profesa Jay ameeleza sababu za kuiita albam yake ‘The Icon’ kama msanii mkongwe ambaye bado anang’aa katikati ya wasanii wengi chipukizi.
“Nataka nitengeneze albam inaitwa The Icon, kwamba Profesa Jay alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo kwa sababu huu ni mgodi unaotembea.” Profesa Jay ameiambia tovuti ya Times Fm.
Amesema jina hilo la albam ‘The Icon’ linatokana na jina alilopewa na kiongozi wa Kwanza Unit, Zavara aka Chief Ramso. Amesema Zavala alimfananisha na  Vasco Da Gama, Mreno ambaye aliweka historia ya kuwa mtu wa kwanza kutoka Ulaya kuingia India kwa njia ya bahari katika karne ya 14.
“Yule kiongozi wa Kwanza Unit ya zamani ile, Chief Ramso yule alinipa jina la Vasco Da Gama. Vasco Da Gama ni yule jamaa alionekanaga zamani akizunguka huku na huku, alikuwa yeye ni mfanyabiashara.” Amesema Profesa Jay.
Hata hivyo hakuitaja tarehe au mwezi anaotarajia kuiachia albam hiyo na kueleza kuwa watanzania wajue bado ana vitu vingi kwa ajili yao na hajavunja kibubu..

0 Response to "PROFESA JAY AFANANISHWA NA VASCO DA GAMA"

Post a Comment