Ngoma za ‘Bunyerobunyero’ zapigwa STOP na jeshi la polisi

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema itawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa klabu za usiku zinazokiuka maadili kwa kuruhusu klabu zao kupiga ngoma ya ‘bunyerobunyero’.KovaWaandishiNgoma hiyo iliibuka na kuwa maarufu hasa jijini Dar es Salaam baada ya Polisi kupiga marufuku ngoma ya ‘kantangaze-kigodoro’ na ‘khanga moko’.Onyo hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kanda hiyo, Suleiman Kova wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema ngoma hiyo imeibuka karibuni na inaenda kinyume na maadili ya Kitanzania.Alisema ngoma hizo hazina tofauti kubwa na vigodoro isipokuwa wahusika wa ‘bunyerobunyero wametofautisha maeneo ya kupinga ngoma hiyo ambayo ni kwenye klabu za usiku tofauti na vigodoro ilikuwa ikipigwa mitaani.“Tutahakikisha kwa kushirikiana na halmashauri za miji pamoja na polisi kuhakikisha hizi ngoma za ‘bunyerobunyero’ tunazipiga marufuku, kwasababu zinakiuka maadili,” alisema Kova.Alisema Polisi imetoa onyo mara nyingi kuhusu ngoma hizo na kwamba hatua inayofuata sasa ni kuwakamata wachezaji na wahudhuriaji wa ngoma hizo pamoja na kuwakamata wamiliki wa klabu hizo na kuwapiga faini na kuzifungia klabu hizo.“Onyo hili linatolewa kwasababu hizi ngoma zimeenea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam,” alisema.Kamanda Kova alisema ngoma hizo zimetawaliwa na udhalilishaji wa hali ya juu jambo linalochangia kuporomoka kwa maadili, hivyo hawatalifumbia macho.“Uchunguzi kwasasa unafanyika na endapo itabainika ngoma hizo kuendelea kuchezwa basi Jeshi la Polisi na halmashauri za miji zitachukua hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuzifungia klabu hizo kwasababu zinakiuka taratibu za leseni,” alisema.

0 Response to "Ngoma za ‘Bunyerobunyero’ zapigwa STOP na jeshi la polisi"

Post a Comment