MOVIE SUPERSTAR LUPITA NYONG’O NA FAMILIA YAKE KUTUA TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014

DSC_0082
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo.
Lupita-Nyong-o-729-620x349
Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba
Tukio kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa  kwenye viunga vya Zanzibar  na nchi nyingine duniani katika tamasha hilo la 17, ni ujio wa msanii wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o, atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za ZIFF mwaka huu.
Lupita ambaye ametwaa tuzo za Oscar na nyingine nyingi na kupelekea kutikisa Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye tamasha hilo huku akitarajiwa kuambatana na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake.
Prof. Mhando amesema tayari wazazi wote wawili wa Lupita akiwemo Dorothy na Peter Anyang’ Nyong’o, watakuwapo kwa siku zote 10 kwenye tamasha hilo huku Lupita mwenyewe akiahidi kuangalia uwezekano wa kuhudhuria japo katika utoaji wa tuzo kama ratiba za shughuli zake hazita mbana.
Prof. Mhando alisema Lupita ni zao la ZIFF na ndiyo iliyomfungulia mwanya wa kujulikana na baadaye alienda kusoma zaidi masuala hayo ya filamu, ambapo alishiriki ZIFF 2007 kama Volunteer.
Mara nyingi staa huyo amekua akihudhuria matamasha na halfa mbalimbali za utoaji wa tuzo na zawadi zingine huku akiwa ameambatana na wazazi wake wote wawili.
 Lupita mbali na tuzo hiyo ya Oscar, kupitia filamu ya ‘12 Years a Slave’ pia  filamu hiyo imempatia tuzo mbalimbali zikiwemo: tuzo ya Steve McQueen kama mwigizaji mwenye mvuto, mwigizaji bora wa kike aliyeshirikishwa, ‘Academy Award’, ‘Screen Actors’ Guild Award’, ‘NAACP Image Award’, ‘Independent Spirit Award’, ‘Broadcast Film Critics Association Award’,  na nyingine nyingi.
Genevieve-Nnaji-Cover
Genevieve Nnaji.
Mbali na Lupita, katika kuongeza utamu wa tamasha hilo, mastaa wengine nguli wa Afrika kwa mwaka huu wanaotarajiwa kuwapo katika ushuhudiaji wa utoaji wa tuzo hizo ni pamoja na muigizaji na mwanamitindo nyota wa Nigeria, Genevieve Nnaji.
Wengine ni Amr Waked (Misri),  Faouzi Bensaidi (Morocco),  Nadia Buari, Richard Mote Damijo ‘RMD’,  John Dumelo, Desmond Eliot na  Florence Masebe.
DSC_0067
DSC_0137DSC_0021

0 Response to "MOVIE SUPERSTAR LUPITA NYONG’O NA FAMILIA YAKE KUTUA TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014"

Post a Comment