YALIOJILI UTOAJI WA TUZO ZA WATU 2014

Tuzo za watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards zimetolewa Ijumaa hii kwenye ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Jumla ya vipengele 11 vilikuwa vinashindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na trophy. Host wa tuzo hizo alikuwa mtangazaji mkongwe wa radio, Jimmy Kabwe.
King Majuto akifurahi mara baada ya kupokea Tuzo yake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kipengele cha Msanii Bora anayependwa wa Kiume.
Jimmy Kabwe akiendelea Kutangaza

Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited, Evance Stephen (Kushoto) akiwa na Msanii Bora wa Kike katika Tuzo za Watu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu mara baada ya Kutangazwa Mshindi wa Kipengele cha Msanii Bora wa Kike anayependwa.
Faraja Kota Nyalandu (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mrs Mengi Kylin
Babu Tale akipokea tuzo ya Video bora Kwa Niaba ya Msanii Diamond Ambae hakuwepo katika Utoaji Tuzo hizo. Nyimbo ya My Number one ya Diamond Ndio Nyimbo inayopendwa
Mustafa Hassanali (Kulia) akimkabidhi Mwakilishi wa Lady Jay Dee Tuzo ya Video Bora ya Yahaya
Wadau wakifuatilia Sherehe za Utoaji Tuzo hizo zilizofanyika jana katika Ukumbi uliopo katika hoteli ya Serena
Watangazaji wa Clouds Media , Adam, Millard Ayo na B12 wakijadiliana jambo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za Watu.

Akiwashukuru Wadau waliompigia kura na kumpa sapoti
Salim Kikeke kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC akiwashukuru wadau wake waliomuwezesha kushinda Tuzo

WASHINDI

1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM

2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM

3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number – Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee

09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto

10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael

11. FILAMU INAYOPENDWA.

 

0 Response to "YALIOJILI UTOAJI WA TUZO ZA WATU 2014"

Post a Comment