NYOTA NDOGO AELEZEA KWA NINI ANAHOFIA VIDEO YAKE YA "UTUPU" INAWEZA KUVUJA, NA KILICHOMTOKEA HADI AKAREKODIWA AKIWA MTUPU

Muimbaji kutoka Mombasa, Kenya Nyota ndogo amejikuta katika hali ya wasiwasi baada ya kukutwa na mkasa wa karne hivi karibuni. 

Nyota ameelezea kilichomkuta baada ya kuingia kwenye chumba cha hoteli ili abadili nguo, na kwa bahati mbaya alivua nguo zake mbele ya kioo cha chumba hicho bila kujua kioo hicho upande wa nje kinaonesha live bila chenga. 

Kupitia akaunti yake ya Facebook Nyota Ndogo ameelezea kilichomsibu: 'yani nimekwenda show.nikapewa chumba chakubadili nguo.nimevua nguo zote najipaka mafuta pole pole kumbe najiangalia kwa kioo kumbe upande wapili naoneka kila kitu.yani nimekosa amani"aibu nilio iona mungu ndio anajua.sijui wamechukua video..haya ngoja tusubiri". 
 nyota1
Hata hivyo Nyota amewapunguza wasiwasi mashabiki wake walio comment kumpa pole kwa kusema alibakiwa na nguo za ndani wakati hayo yanatokea. "hapana nilibakisha cha ndani na nyonyo ilikua na nguo pia.kitu sielewi ni alienipeleka kubadili nguo ina maana hakujua nje naonekana?maana aliambia kioo hiki jiangalie mpaka miguu."
 nyota2

Nyota ameamua kuwapa taarifa mashabiki wake mapema ili endapo kama kuna aliyerekodi na video ya tukio hilo ikisambaa watu wafahamu kilichotokea.

0 Response to "NYOTA NDOGO AELEZEA KWA NINI ANAHOFIA VIDEO YAKE YA "UTUPU" INAWEZA KUVUJA, NA KILICHOMTOKEA HADI AKAREKODIWA AKIWA MTUPU "

Post a Comment