Mwandishi maarufu aanzisha dini yake kupinga wanaume, atangaza kuwa Mungu wa dini hiyo.

Mwandishi maarufu aanzisha dini yake kupinga wanaume, atangaza kuwa Mungu wa dini hiyo 
Mwandishi maarufu wa vitabu ambaye aliwahi kushinda tuzo nyingi, Kola Boof ambaye aliwahi kukiri kuwa mfanyakazi wa Osama Bin Laden ameibuka na jipya kwa kutangaza dini yake.
Kola Boof ametangaza kupitia Twitter kuwa amenzisha dini yake mpya inayoitwa The Womb kwa lengo la kuwasaidia wanawake na kupingana na kile anachokiita mfumo dume kwenye vitabu vyote vya dini.
Katika utetezi wake ameeleza kuwa anaamini vitabu vya dini kama Biblia imeandikwa na mwanaume hivyo ni lazima ingemkandamiza mwanamke. Ameeleza kuwa hataki kabisa kuamini kama kuna Mungu wala dini zilizopo hazimshawishi hivyo ameamua kuja na yake na yeye ndiye Mungu wa dini hiyo.
Lengo kubwa la dini yake anaeleza kuwa ni kumfanya mwanamke awe huru na suala la mapenzi na viungo vyake vyote bila kumtegemea mwanaume.
Hata hivyo ameeleza kuwa yeye sio mhubiri na hatamshawishi mtu kujiunga na dini yake, dini yake itakuwepo tu.
Katika hatua nyingine, mwandishi huyo ambaye yuko chini ya uangalizi wa Marekani tangu akiri kuwa msaidizi wa Osama Bin Laden mwaka 2002 alieleza kuwa aliamua kukubali kuwa ni msaidizi wa Osama baada ya Marekani kumtishia kuwa wangemfukuza watoto wake Marekani endapo asingekiri.
Kola Boof amewahi kutajwa na CNN kuwa mwanamke mtata (controversial) zaidi duniani.
Wazazi wake waliuawa mbele yake baada ya wao kuzungumzia masuala tata juu ya Sudan.
  KOLA BOOF (Official) @KolaBoof
I started my own religion, it's called THE WOMB. I don't want Men's religions. @Flowfy
  KOLA BOOF (Official) @KolaBoof
The ONLY reason I admitted to Bin Laden affiliation after Guardian outed it...was bec. U.S. threatened to deport my sons. @MalaikaAdero

0 Response to "Mwandishi maarufu aanzisha dini yake kupinga wanaume, atangaza kuwa Mungu wa dini hiyo."

Post a Comment