MLIPUKO WA BOMU ULIOUWA WATU 48 KENYA

Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, Takribani watu 48 wameuwawa   nchini  Kenya  baada ya kikundi kinachodaiwa kuwa cha wapiganaji wa kiislamu kushambulia hoteli na kituo cha polisi katika mji wa Pwani wa nchi hiyo. 
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walishuhudia mapigano ya risasi yaliyodumu kwa saa kadhaa pamoja na majengo kuchomwa moto.
Mji huo uko karibu na kisiwa cha Lamu ambacho ni maarufu kwa hoteli nzuri za kitalii.
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2011 wakati vikosi vyake vya kijeshi vilipoingia Somalia kwa ajili ya kusaidia kupambana na wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab

0 Response to "MLIPUKO WA BOMU ULIOUWA WATU 48 KENYA"

Post a Comment