MBUNGE JOSHUA NASSARI NA ANANDE NNKO WAMEREMETA KWENYE KANISA LA PENTEKOSTE KILINGA,MERU

Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete mkewe Anande Nnko.
Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda mfupi baada ya kuvishana.
Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na hapa maharusi wakitia saini katika vyeti yao.
Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete mumewe Joshua Nassari.
Msafara wa gari chache majira ya saa 2:30 ulianza safari katika viwanja vya Usa-River ambako gari za maharusi zilikuwa zikipambwa mdogo mdogo zikapanda Kilima zikiwa na maharusi Joshua Nassari na Anande Nnko safari ilikuwa ni kanisa la Kipentekoste la Kilinga,Meru tayari kwa ajili ya Ndoa.
Hatimaye Bw Harusi Joshua Nassari anateremka katika usafiri wake aina ya Range Rover muda mfupi baada ya kufika katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu kama kwa Mchungaji Babu.
Wageni mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ya ndoa mmoja wapo ni huyu ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai(katikati)
Bibi Harusi Anande Nnko alikuwa ni mwenye furaha kila wakati ,"Full Tabasamu."
Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu walikuwa wamevalia mavazi nadhifu aina ya suti wakingojea ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la Kilinga.
Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi Anande Nko.
Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX.
Kisha Maharusi wakapongezana.
Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT) David Batenzi.
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada hiyo (hawapo pichani)

Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa kwanza)
"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.
Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.
Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.
Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka zao katika kapu la sadaka.
Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.
Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani.

0 Response to " MBUNGE JOSHUA NASSARI NA ANANDE NNKO WAMEREMETA KWENYE KANISA LA PENTEKOSTE KILINGA,MERU"

Post a Comment