Lupita yawanyamazisha waliomkosoa kuwa kisura wa kampuni yenye bidhaa za kujichubua

 Picha ya Lupita yawanyamazisha waliomkosoa kuwa kisura wa kampuni yenye bidhaa za kujichubua
Baada ya kutoka tangazo kuwa Lupita Nyong’o atakuwa kisura wa kwanza mweusi kwenye bidhaa ya Lancome, wengi walianza kumkosoa kwa uamuzi wake kwa kuwa kampuni hiyo ina bidhaa za kujichubua ngozi.
Hata hivyo, picha ya kwanza ya kampeni ya Lupita kwa bidhaa tofauti za kampuni hiyo zimewanyamazisha walioanzisha mgogoro huo. Lupita ameitangaza Tiente Idole Ultra 24H.
Sasa kampuni hiyo imetangaza ngozi nzuri ya mrembo Lupita Nyong’o bila kuwa na dalili za kujichumbua. Huenda ikawashawishi wateja wao kuachana na mpango wa kujichubua kwa kuwa black is beauty.

0 Response to "Lupita yawanyamazisha waliomkosoa kuwa kisura wa kampuni yenye bidhaa za kujichubua "

Post a Comment