kKANISA LACHOMWA MOTO UJIJI KIGOMA


Watu wasiojulikana wamechoma moto kanisa la Pentekoste Christian Gospel Revival Assemblies, lililopo eneo la Masanga katika manispaa ya Kigoma/Ujiji majira ya usiku.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea na uchunguzi kubaini wahusika
Hili ni kanisa la pili kuchomwa moto mjini Kigoma baada ya tukio la mwaka jana la kanisa la Muungano wa makanisa ya pentekoste Tanzania (MMPP) katika eneo la Butunga kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

0 Response to "kKANISA LACHOMWA MOTO UJIJI KIGOMA"

Post a Comment