Jay Z amemtimua bodyguard aliyedaiwa kuchepuka na Beyonce!?..

 Jay Z amemtimua bodyguard aliyedaiwa kuchepuka na Beyonce!?
Tuhuma za Beyonce kumsaliti Jay Z na kutoka na mlinzi wake aitwae Julius De Boer zilisambaa mwezi uliopita huku likiwaacha mashabiki wao midomo wazi.
Katika hali inayoonekana kuwa Jay Z amezifanyia kazi kwa msisitizo zaidi, Beyonce ameonekana mitaani akiwa mlinzi mwingine ambaye hakufahamika huku wengi wakiuliza nini kimemkuta Julius? Au ndio katimuliwa kabisa?
Taarifa za awali zilidai kuwa Jay Z baada ya kuona Julius yuko karibu sana na Beyonce huku ikielezwa kuwa mara nyingi waliposafiri pamoja kwenda ziarani, walikaa hotel moja na mlinzi huyo alikuwa anaingia hata chumbani kwake.
 Inadaiwa kuwa Jay Z aliamua kumfukuza kazi Julius lakini Beyonce aliweka ngumu.

0 Response to "Jay Z amemtimua bodyguard aliyedaiwa kuchepuka na Beyonce!?.."

Post a Comment