BATULI AWANG'AKIA WANAOTABILIA VIFO WASANII

STAA wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amesema kama kuna mtu yeyote anahusika na vifo vya wasanii katika ushirikina basi anajisumbua, kwake hawafui dafu.
STAA wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’
Batuli ameiambia Bongowood kuwa, hana uhakika kama wasanii hao vifo vyao vinatokana na mkono wa mtu kama minong’ono iliyoenea lakini kama kuna mambo ya nguvu za giza yanaendelea, kwake watashindwa sababu anamtegemea Mungu.
“Sitaki kuamini sana kama hali hii inatokana na nguvu za giza lakini kama kuna mambo ya ushirikina yanatendeka basi kwangu watashindwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu,” alisema Batuli.

0 Response to "BATULI AWANG'AKIA WANAOTABILIA VIFO WASANII"

Post a Comment