Audio: Dayna Nyange afunguka kuhusu uhusiano wake na Nando.

 Audio: Dayna Nyange afunguka kuhusu uhusiano wake na Nando
Mwimbaji wa Nivute kwako Dayna Nyange amezungumzia uhusiano wake na mshiriki wa Big Brother Africa, Ammy Nando baada ya kuonekana katika picha kadhaa wakiwa katika poz tata.
Dayna amefunguka jana kupitia The Jump Off ya 100.5 Times Fm na kueleza ukaribu wao na kinachoendelea.
“Jamani Nando ni rafiki yangu, hakuna kitu serious,  he’s just a friend tu basi.Sijui nisemeje, ni watu ambao tumefahamiana si kwa muda mrefu sana lakini tumeshibana so imekuwa hivyo tumekuwa karibu mara kadhaa. Haipiti muda mrefu bila kuonana kwa hiyo mara nyingi tunakuwa wote. Ninamkampani kwenye issue zake na yeye ananikampani pia mimi, ni watu ambao tumekuwa karibu sana kwa kweli.” Dayna ameiambia The Jump Off ya Times Fm.
Alipoulizwa kuhusu picha zao zinazoonekana kwenye Instagram ambazo zinaongea zaidi ya urafiki, alifunguka:
“Yeah...sasa mtu na rafiki yake si mnapiga picha mnakuwa free jamani…hivyo (kicheko).”
Hata hivyo, Dayna amesema kuna kitu ambacho wanakifanya pamoja na kitakapokuwa tayari watu watafahamu.

0 Response to "Audio: Dayna Nyange afunguka kuhusu uhusiano wake na Nando."

Post a Comment